Habari

Akamatwa kwa kufukua maiti ya mtoto, kuipika mchuzi na kuila

Nchini Pakistan Polisi wamewakamata wanaume wawili kwa makosa ya kuiba maiti ya mtoto kutoka kaburini na kisha kumla. Wawili hao Arif Ali na kakake Mohammed Farman Ali waliachiwa huru baada ya kuwa jela kwa miaka miwili kwa kula nyama ya binadamu.

140414145055_mohammad_arif_ali_512x288_ikrampiracha_nocredit

Wakaazi hao wa kijiji cha Daryabn Khan jimbo la Punjab walikamatwa mwaka 2011 kutokana na kosa hilo huku wameonekana kuwa na tamaa kubwa ya mchuzi wa nyama ya binadamu. Polisi walisema kwamba walipata kiwiliwili cha maiti ya msichana mdogo kikiwa bila miguu na mikono. Wawili hao walikiri kwamba walikua wanapika mchuzi wa nyama ya viungo hivyo na kuvila.

Walishtakiwa kwa makosa ya kuharibu kaburi kwani nchini Pakistan hakuna sheria inayozungumzia hatia ya mtu kumla mwenzie. Punde baada ya kuachiwa nguvu Arif Ali aliambia BBC kwamba anajutia makosa hayo na kwamba hatarudia tena.

Hata hivyo punde si punde polisi wamesema waliitwa na majirani ya jamaa huyo wakilalamikia uvundo mkali kutoka kwa nyumba yake. Walipoingia chumbani humo Lo ! wakapata kichwa cha mtoto na kiwiliwili hakijulikani kililiwa au kapotelea wapi.

Arif Ali tena amekamatwa kwa mara ya pili na msako unaendelea kumsaka kakake. Polisi wanaamini ndugu hawa walifukua maiti ya mtoto ambaye kichwa kilipatikana ndani ya makaazi yao. Wawili hao waliwahi kuoa na hata wakajaliwa na watoto, hata hivyo wake zao waliwatoroka kabla yao kwenda jela kwa kisa cha awali.

Source:BBC

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents