Burudani

AIM ya Navy Kenzo yamfanya Rama Dee ashindwe kuachia albamu yake mpya

Muimbaji wa R&B nchini, Rama Dee, amedai kuwa albamu mpya ya Navy Kenzo, Above In A Minute (AIM) imekatisha mipango yake ya kuachia albamu mapema.

Kupitia mtandao wa Instagram, Rama Dee amesema kutokana na albamu hiyo kuwa kali na ubora wake mzuri ndio sababu iliyomfanya abadili tarehe ya kuachia albamu yake.

Kupitia mtandao huo, muimbaji huyo ameandika:

Baada ya kusikiliza hii album nimebadilisha tarehe ya utoaji wa album yangu! Album ipo kali sana @nahreel You did my friend, Good on you???????? please nenda nunua hii album ni nzuri sana ipo kwenye kiwango kizuri kabisa haina ujanja ujanja!

Naye Nahreel hakusita kupokea credit hizo, amjibu kwenye mtandao huo kwa kuandika, “God Bless You @rama_deetz Good Music Alive.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents