Burudani

Afande Sele: Leo ni birthday ya Tunda, napata wakati mgumu mama yake hayupo

Rapper kutoka Morogoro Afande Sele amesema leo ikiwa ni siku ya kuzaliwa ya mwanae Tunda, anapata mtihani wa kwanza wa kusherehekea siku hiyo wakati mama yake hayupo tena duniani.

afandesele

Akizungumza na Bongo5 leo ,Afande Sele amesema ingawa alikuwa na matatizo na mke wake wakati yupo hai lakini bado alikuwa ni kiungo kibubwa kwenye familia yake.

“Leo ni birthday ya mwanangu Tunda, leo katimiza miaka 13 nataka niende shule kumsalimia lakini ni birthday ya kwanza bila mama yake,” amesema Afande.

“Napata wakati mgumu sana hata kusema siwezi kwa sababu siku zote mzazi mwenzangu alikuwa mtu ambaye anafanya kazi kubwa, matatizo ya kawaida yapo mpaka anaondoka duniani hatuko sawa lakini masuala ya watoto alikuwa yupo mbele sana kusema ukweli
Alikuwa anajali sana watoto wake, anafuatilia hatua moja hadi nyingine, kipindi hiki ambacho nipo peke yangu yeye hayupo najikuta kwamba navaa kofia ambayo sikutegemea. Nimeona kwamba uzito wa tukio la kuondoka kwake ni mkubwa kuliko nilivyokuwa nikifikiria mwanzoni.”

“Leo nilikuwa nina kazi nifanye Chalinze na mpaka sasa kazi hiyo ninayo lakini siwezi kwenda kwenye kazi moja kwa moja bila kwenda kumuona mtoto shuleni kwa sababu alizoea siku kama ya leo mama yake ataenda mapema sana, baba asipomuona anajua yupo mtaani anatafuta maisha yetu lakini mama yupo mjini. Sasa leo hii mama yake hayupo, nakuwa mimi ndio baba ndio mama, na ndio kila kitu kwahiyo najikuta na wakati mgumu sana kuona kwamba katika mwezi ambao nimempoteza mama mtu na ndo mwezi ambao mtoto wangu alizaliwa, leo ni birthday ya mwanangu Tunda, napata wakati mgumu sana na mama yake hayupo,” amesema Afande.

Mama Tunda alifariki dunia usiku wa August 14 mkoani Morogoro na kuzikwa katika makaburi ya Kolla yaliyopo mkoani humo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents