Burudani

Afande Sele azungumzia ujio wa nyimbo mbili mpya

Afande Sele anatarajia kuachia nyimbo mbili kwa mpigo.

Afande-Sele-nzuri_full

Rapper huyo ameiambia Bongo5 kuwa uamuzi wa kuachia nyimbo mbili ni kukata kiu ya mashabiki wake waliokuwa wakisubiria muziki wake.

“Kuna nyimbo mbili bado zipo kwenye maandalizi, moja inaitwa Mfungwa. Hii ni nyimbo ambayo ndani nitazungumzia matatizo yanayowakuta wafungwa, wafungwa wanavyonyanyasika,” amesema Afande.

“Na wimbo wa pili utazungumzia pia maisha fulani jinsi tunavyoishi kwa visasi, unakuta dereva wa gari ana kisasi na muuza mafuta, muuza genge ana kisasi na muuza nyanya. Kwahiyo ni wimbo fulani ambao utahitaji kutuweka sawa ili kuishi kwa pamoja bila kuwa na visasi.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents