Michezo

Adebayor amshutumu mama yake kwa uchawi

Mchezaji wa klabu ya Tottenham, Emmanuel Adebayor, amedai kuwa mama yake amekuwa akitumia uchawi kujaribu kumharibia kazi yake.

141121123944_adebayo_512x288_bbc

Taarifa zimedai kuwa mama huyo tayari ameondoka katika nyumba ya familia huku dada yake Adebayor akikiambia kituo kimoja cha redio mjini Accra kuwa Adebayor ndiye aliyemfukuza.

Mchezaji huyo wa zamani wa Arsenal anadai kuwa mama yake aliondoka mwenyewe na kwamba hawana mawasiliano yoyote kati yao kwa kuwa amekuwa akitumia uchawi kutaka kumharibia kazi yake.

“Ninawezaje kuzungumza na mama ambaye yeye na dada yangu wamekuwa wakijaribu kuniloga,” alihoji Adebayor. Kiwango cha mchezaji huyo kimeendelea kushuka na kuwafanya Tottenham wafikirie kumpiga chini.

Related Articles

One Comment

Leave a Reply

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents