Burudani

Adam Juma: Vifaa tutanunua Inshallah, ila nasisi tutaanza kutangaza bei mnazotulipa. Ni baada ya kauli aliyoitoa Ommy Dimpoz

Kauli ya Ommy Dimpoz aliyoitoa siku mbili zilizopita akishauri wadau wajitokeze na kuwekeza zaidi katika kununua vifaa vya kisasa ili wasanii wasipate sababu ya kwenda kushoot video zao nje, imewafanya madirector nao kutoa yao ya moyoni.

AJ

Kauli ya Ommy Dimpoz imetokana na maswali ambayo watu wengi wamekua wakihoji kwanini wasanii wengi sasa hivi wanaamua kwenda kushoot video zao nje na kwa gharama kubwa ili hali inaaminika hapa nyumbani bado kuna maeneo mengi na mazuri ya kufanyia video ambayo hayajatumika.

Baada ya Nisher kuzungumza na kuwatupia lawama wasanii kuwa wanawadharau madirector wa bongo, Adam Juma wa Visual Lab na yeye ametoa ya moyoni kuhusu kauli hiyo ya Dimpoz, kupitia Instagram ameandika:

“Hahahahahahhahahahahahaha vifaaa tutanunua inshallah, ila sasa nasisi tutaanza kutangaza bei mnazotilipa! Sijawahi kulipwa zaidi ya mil 3.5 na msanii yoyote tanzania km yupo aje ntampa video 10 buree. @rehemavisuallab @nisherbybee @jerrymushalastudios @hefemi @meckykaloka # niggarstalkingshit#mnanitibuasasa#noneducatedniggasoncrack#.”

Director Jerry Mushalla na yeye alicomment kwenye post ya Adam:
“Most Musicians like to blog and talk too much.. But when it comes to actual payments they don’t pay… @adamjumanxl I wish directors woote mngekuwa Na msimamo Wa pamoja @hefemi @nisherbybee @abas_adam @travellah”.

Nisher na Adam Jiuma

Na hiki ndicho Nisher alichokisema wiki hii kuhusu swala hilo:

“Mi sipati logic wasanii wanavyosema wanaweza kulipa sijui milioni za hela wapi…mi napigiwa simu na wasanii wakubwa lakini kila anaekupigia anasema mi sina hela lakini mi naweza kukugharamia chochote unachotaka tushoot video.

Unaanzaje na kauli halafu na wakati mi nasoma kwenye Internet kwamba umelipa sijui kiasi gani gani gani kwenye video flani flani, nafikiri video ya Ben Pol juzi tu ambayo tuliifanya ‘Unanichora’ labda ndio video niliyopata hela nyingi kwa kiasi flani kwa sababu video iligharimu karibu milioni 10 hivi. Mi nadhani tunachukuliana poa na kudhariana kiukweli.

Kwa Mfano ukinilipa milioni 5 au 10, una uhakika kwamba hela hiyo hiyo itatumika kusambaza kazi yako[…] kufanya kila kitu. Vyombo vipo cranes nini, cranes zenyewe za kukodi kwa siku laki 5, camera zipo za kukodi Red Camera unaambiwa labda dola 800 kwa siku, nani atakupa hiyo hela? Hivi vitu vinakatisha tamaa wasanii hawatukubali wanatuona kama hatujui.”

Ommy Dimpoz

Hiki ndicho alichokisema Ommy Dimpoz wiki hii na kuwafanya madirector nao kuamua kufunguka:

“Biashara ya video ishaingia ushindani, kwahiyo kuna haja ya kuwekeza kwenye vifaa, m i nauhakika hapa mtu ana mavifaa kibao unaenda kushoot Lushoto huko noma, wazungu wenyewe watauliza umeshoot wapi. Tuna maeneo kibao Zanzibar wapi wapi wapi ya kushutia, sio kwamba hatuna maeneo, maeneo tunayo lakini hatujawa na vile vitu. Kwahiyo ndo maana hata mtu pia unafikiria ah sijui nishoot Zanzibar, lakini unawaza kumchukua labda GodFather au nani kumleta huku Tanzania ndio mziki.

Halafu mtu utakapoleta vifaa hivyo nauhakika hautaishia kwenye video tu, kuna matangazo, utakodi utafanyaje…Watu lazima waelewe kitu kimoja kwamba hakuna mtu anaependa kujitia gharama kama kuna uwezo wa kuepuka gharama, sio ufahari mi nina vitu vingi vya kufanya sio kwamba nataka tu nikalipe dola elfu 30 kushoot video wakati nina uwezo wa kuokoa hiyo hela labda kulipa dola elfu 15 au elfu 10.

Wadau wanatusikia sie ndio wasanii wenyewe tunasema kwamba muziki unalipa mnaona sasa hivi vijana wenu wanapata shilingi mbili tatu, hizo shilingi mbili tatu mtagawana nao vipi kuliko kwenda kuwapa watu wengine huko nje ya nchi.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents