Habari

ACT Wazalendo wamtega CAG kubaini suala la upungufu wa chakula nchini

Chama cha wananchi ACT – Wazalendo kimemwomba Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kufanya ukaguzi maalumu katika maghala ya chakula kubaini ukweli juu ya kuwapo upungufu wa chakula nchini.


Katibu wa Itikadi, Mawasiliano ya Umma na Uenezi wa chama hicho, Ado Shaibu.

Akizungumza na wanahabari Jumatano hii, Katibu wa Itikadi, Mawasiliano ya Umma na Uenezi wa chama hicho, Ado Shaibu, alisema kinapinga propaganda hiyo ya kusambaza tani milioni 1.5.

“Tusiishie tu kwamba chakula kipo pungufu, sisi tunaendelea kufuatilia, tunazo taarifa kwamba kulikuwa na ubadhilifu kulikuwa na harufu ya ufisadi katika ugawaji wa vibali wa kuuza chakula nje, kwahiyo tunamuomba mkaguzi mkuu wa mahesabu ya serikali akague achunguze chimbuko la uhaba wa chakula katika maghala yetu,”alisema Shaibu.

“Tuna imani kabisa moja ya hoja atakazo kuja nazo na hitimisho atakalo kuja nalo ni ugawanyi mbovu wa vibali vya chakula, na kama hilo likidhihirika basi hatua zichukuliwe, tunaamini kwamba ofisi ya CAG itatekeleza wajibu wake, tuna imani hiyo na ndiyo maana na ndiyo maana tumeipa changamoto hiyo kwasababu ofisi ile ni huru isiyopaswa kuingiliwa,katika kutekeleza majukumu yake.”

Siku kadhaa zilizopita Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dk. Charles Tizeba, alisema hadi kufikia Januari 12, mwaka huu, NFRA ina akiba ya tani 88,152 za mahindi na kusisitiza kuwa hali ya chakula nchini inaridhisha.

BY: Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents