Habari

Abdul Kiba: ‘Nimechoka kuishi kwenye mapenzi ya utumwa’, azieleza hisia zake kwenye wimbo mpya

Msanii na mdogo wake Ali Kiba, Abdul Kiba anarajia kuachia ngoma mpya iitwayo ‘Mapenzi ya Utumwa’ ambayo ameimba jinsi alivyoumizwa mapenzi.

Abdul Kiba

Akiongea na Bongo5, Abdul amesema ameamua kurudi upya kwa style ya mapenzi baada ya kuumizwa kwa muda mrefu na kuamua kutengeneza ngoma ili kufikisha ujumbe kwa wengine ambao wameshaumizwa kama yeye.

“Nakuja na mapenzi kitu ambacho kinaumiza wengi ambapo hata mimi nimeshaumizwa sana, hakuna mtu asiyependa kuona anapendwa sana ila unakuta mtu akigundua anapendwa anazingua ndiyo maana nikafanya ‘Mapenzi ya Utumwa’.Hii ngona itakuja pamoja na video na inatengenezwa Chinese Record pale Mikocheni, chini ya producer Abby Daddy,” alisema.

Pia Abdul aliomba mashabiki wampokee tena kwenye wimbo mpya.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents