Burudani

Abdallah ‘Dulla’ Ambua wa EATV aliwahi kuwa fundi wa viyoyozi!

Mtangazaji wa kipindi cha Planet Bongo cha EATV na EA Radio, Abdallah ‘Dulla’ Ambua ana ‘relate’ moja kwa moja na wimbo wa Drake ‘Started From The Bottom’ kwakuwa ustaa alionao sasa haukupatikana kirahisirahisi.

ambua

Akielezea historia yake kwa ufupi leo kupitia kipindi cha East Africa Breakfast, mtangazaji huyo alisema kabla ya kuwa mtangazaji alikuwa fundi mzuri wa viyoyozi na moja ya kazi kubwa alizofanya ni kufunga viyoyozi vya hoteli ya Hyatt Regency (zamani Kempinsk).

Cha kufurahisha zaidi ni kuwa katika kazi hiyo aliwahi kuitwa kwenda kurekebisha AC za East Africa Radio na katika wakati mmoja mtangazaji wa zamani wa Planet Bongo, Salama Jabir alimsaidia kumshikia mlango wakatia akipitisha vifaa.

Ambua anasema kuwa kazi hiyo haikuwa ikimlipa na alikuwa akiingiza takriban 2,500 kwa siku. Amedai kuwa kipaji chake cha kutangaza kiligunduliwa na kaka yake Said Ambua ambaye pia ni mtangazaji wa Uhuru FM.

Anadai kuwa kuna siku aliichukua tape recorder ya kaka yake iliyokuwa ndani na kuichezea kwa kuhoji watu mtaaani na kaka yake aliposikia kilichomo ndani, alivutiwa na uwezo wake mdogo wake hivyo kumpigia debe apate kazi kwenye kampuni ya matangazo ya Intergrated ambao bila kusita walimchukua.

Alifanya kazi ya kutangaza bidhaa mbalimbali kwenye magari ya promotion kabla ya kusikia tangazo kuwa EATV wanahitaji mrithi wa kipindi cha Planet Bongo. Dullah alishiriki na kuingia top 10 huku akichuana na watangazaji wengine wakiwemo Ezden Jumanne aka The Rocker na Allan Lucky na bahati kumwangukia yeye.

Kwa sasa Dullah ameoa na ana watoto wawili wa kike.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents