Burudani

50 Cent awafungulia mashtaka mawakili wake, ataka alipwe $30m

50 Cent anataka malipo yake ya fidia aliyomlipa Lastonia Leviston.

Kwa mujibu wa mtandao wa The Wrap, rapper huyo amewafungulia mashtaka wanasheria wake wawili Reed Smith na Peter Raymond waliokuwa wanasimamia kesi yake dhidi ya Lastonia ya mwaka 2015.

Rapper huyo amewashitaki wanasheria wake hao wa zamani kutokana na kushindwa kusimamia kesi yake iliyokuwa ikimkabili ya kusambaza kanda za picha za uchi za mrembo huyo ambaye aliwahi kuwa mpenzi wa Rick Ross na kupewa amri na mahakama ya kulipa kiasi cha dola milioni saba.

50 Cent ametaka kulipwa fidia ya kiasi cha dola milioni 32 kutokana na kesi hiyo huku fidia ya dola milioni $25 kwa usumbufu aliopata na zingine $7m kwa gharama alizotumia.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents