Burudani

41 Records – Levels za hatari!

41 RecordsNi vigumu sana unapokuwa unataja orodha za majina ya studio ambazo zinafanya vizuri hapa nchini ukataja tatu bila kuitaja 41 Records studio pekee ambayo imeweza kujipatia jina katika kipindi kifupi tangu ianze kupiga kazi hadi kufikia hatua ya kuzifanya baadhi ya studio kongwe kama kufutika katika masikio ya wasanii na wapenzi wa burudani kwa ujumla

41 Records

 

 

 

Ni vigumu sana unapokuwa unataja orodha za majina ya studio ambazo zinafanya vizuri hapa nchini ukataja tatu bila kuitaja 41 Records studio pekee ambayo imeweza kujipatia jina katika kipindi kifupi tangu ianze kupiga kazi hadi kufikia hatua ya kuzifanya baadhi ya studio kongwe kama kufutika katika masikio ya wasanii na wapenzi wa burudani kwa ujumla.

 

 

 

Akizungumza na Bongo5.com The CEO wa 41 Records Lufunyo alisema kuwa “wazo la kuanzisha studio lilikuwa akilini mwake na kulikuwa na kila sababu ya kuwepo kwa lengo hilo na kuhakikisha linatimia kwani mimi ni mwanamuziki mwenye mapenzi ya dhati kabisa na muziki hivyo kuwa na studio ni moja kati ya ukamilifu wa malengo yangu kwani kila nilichokuwa nikikifanya nilijikuta automatic naangukia kwenye muziki”

 

 

 

Lufunyo amedai moja ya watu ambao walikuwa wakimshauri mambo mengi katika muziki na studio kwa ujumla ni pamoja na Prodyuza P-Funk Majani wa Bongo Records “Mchizi alinipa sana moyo wakati naanza Much Respect to him”-Lufunyo.

 

 

 

Katika Studio hiyo unakutana na watendaji kama Prodyuza Dunga a.k.a Ambrose ambaye anatoka katika familia ya wanamuziki nchini Kenya ya Mandugu Digital, akishirikiana na Kijana mdogo saaaaaaana lakini mwenye kufanya maajabu katika kazi za Prodaksheni hapa nchini anayekwenda kwa jina la Lamar, watu hawa ndio husababisha kila kinachosikika hewani kutoka ndani ya Nyumba ya 41 Records.

 

 

 

“Unajua sababu zinazotufanya tukimbiliwa na wasanii wengi kwanza kabisa ni uelewano mzuri na wasanii, Kuambiana ukweli na kupeana ushauri, pia Maprodyuza waliopo hapa 41 wana uzoefu wa hali ya juu sana na kazi yao, hivyo kuna kila sababu ya kufanya vizuri katika anga ya muziki hapa nchini hilo halina ubishi”-Lufunyo.

 

 

 

Bongo5.com ilipata chance ya kufanya mahojiano pia na Prodyuza Ambrose ambaye alisema “ukweli tunajijua kama tunafanya vizuri hatuna budi kuwashukuru wale ambao wanatupa Sapot katika kazi yetu, na hata hivyo malengo na mtazamo wetu ni kufikia katika levo za Billboards na kuangalia hapa karibu kwani tukijipima tunaweza kuona tuna kila sababu ya kufanya vizuri katika hilo na kufika katika levo hizo”

 

 

 

Studio ya 41 Records ina uwezo wa kufanya aina zote za muziki ikiwa ni pamoja na muziki wa asili, lakini bongo5.com ilipohoji kuhusiana na kama wanafanya muziki wa asili mbona hawafanyi muziki wa Bolingo “unajua kutokana na kuku kwa teknolojia ya kiutendaji hasa katika kazi zetu bado hatujaona kama kuna msanii anayeweza kumudu gharama ya kufanya kwani ni kubwa sana na tunaamini iwapo kama atajitokeza atakayekuwa tayari kufanya hivyo tutamfanyia kazi ambayo hataamini masikio yake na ni Hit moja kwa moja” alisema Ambrose a.k.a Dunga.

 

 

 

Mja katika mikakati yao ya kufikia levo za kimataifa ni kujaribu kuzitangaza kazi zao nchi za nje kwa kutuma kazi zao na kufanya kazi na wasanii wa mtoni “Si unacheck Ja Rule kachukua Biti yetu ‘usipime’ ya Rhyno, Loon kaja Bongo kapewa mkono na kakamua ile mbaya na ana mpango wa kurejea tena nchini kwa ajili kufanya kazi tena, halikadhalika tumepiga mkono na Dead Prezz na Kalamashaka pamoja na mengi zaidi yanakuja”-alijipa shavu Ambrose.

 

 

 

Unaweza kuona kijana mdogo Lamar anavyoweza kuumiza vichwa vya wakongwe kadhaa wa hapa nchini kutokana kazi ambazo amekuwa akizifanya ni noma tupu kwani kiukweli kabisa hazilingani na umri wake “unajua kuna kila sababu ya mimi kufanya vizuri sana kwani ukiangalia niko na wataalamu wa shughuli hizi na pia nimkewa na maprodyuza mbali mbali ambao wamekuwa wakinifundisha jinsi ya kuwa prodyuza mkali hivyo acheni tu nifanye vizuri jamani au sio!?-Lamar.

 

 

 

Licha ya shughuli za uedeshaji wa studio 41 Records inatarajia kutoa albam ya kundi lao ukizingatia watu wote pia wana uwezo w kusimama kama wasanii, “kundi letu litakwenda kwa jina la MASHARIKANZ tukiwa na maana ni muunganiko kati ya Tanzania ambayo naiwakilisha Mimi Lufunyo, Kenya inawakilishwa na Ambrose a.k.a Dunga wakati Uganda ikiwakilishwa na Steve Kafaya na mpaka sasa tumeshapiga mikono kadhaa na ngoma tatu tayari zinapatikana hewani nazo ni ‘Makambe, Siku Zijazo na Mitama’ alisema Lufunyo.

 

 

 

Na hii ni moja kati ya miradi ambayo inaendelea chini ya 41 Reecods wakiwa na malengo ya kufanya biashara kimataifa, ambapo wanatarajia kutoka na alba yenye ngoma za kutosha na watapeleka albam ikiwa katika mfumo wa kaseti kwa wadosi na ikiwa katika mfumo wa cd watauza wenyewe kutokana na utaratibu ambao watajiwekea.

 

 

 

Mwisho wanatoa shukrani sana kwa wote ambao wamekuwa wakiwapa sapot ikiwa ni pamoja na watun wa media zote nchini wasanii na baadhi ya wadau wa muziki wa kizazi kipya ambao wamekuwa ni sababu ya kuzidi kuifanya 41 Records kuwa juu.

 

 

 

Bofya hapa kumsikiliza Lufunfyo wa 41 Record akitupa flava za Masharikans live

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents