Picha

36 wauawa kwa shambulio kwenye uwanja wa ndege Uturuki

Shambulio la bunduki na bomu kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Ataturk uliopo kwenye mji mkuu wa Uturuki, Istanbul limesababisha vifo vya watu 36 na kuwaacha wengine zaidi 140 wakiwa majeruhi.

35C4C9F400000578-3664710-image-a-56_1467162412137

Washambuliaji watatu walianza kushambulia kwa bunduki nje na ndani ya uwanja huo wa ndege usiku wa Jumanne hii na walijipua kwa bomu baada ya kushambuliwa na polisi. Waziri Mkuu, Binali Yildirim amesema kuwa dalili za mwanzo zinaonesha kuwa kundi la Islamic State limehusika na shambulio hilo.

35C3FF8B00000578-3664710-Crime_scene_investigators_work_next_to_a_body_after_a_suicide_bo-a-25_1467156133998

Picha kutoka kwenye uwanja huo wa ndege zimeonesha miili iliyofunikwa na mashuka huku vioo na mizigo ikiwa imesambaa kwenye jengo hilo.

35C5B0D600000578-3664710-image-a-1_1467183000399

Rais wa nchi hiyo Recep Tayyip Erdogan amesema shambulio hilo litumike kwa dunia kuwekeza nguvu kubwa katika kupambana na makundi ya wanamgambo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents