Burudani

Exclusive Video: 20 Percent “Sina beef na Afande Sele”

video_20pc
Mshindi wa tuzo za Kili, 20 Percent amesema hana beef la aina yoyote na mfalme wa rhymes, Afande Sele.Miezi kadhaa iliyopita wasanii hao walitupiana maneno machafu redioni ambapo Afande Sele alimshutumu 20 Percent kuwa mhuni kwa kuingia kwenye ugomvi na waandaaji wa tuzo za muziki za Zanzibar.

Kwa upande wake 20 Percent alisema Afande Sele muziki umemshinda ndio maana anaongea maneno ya hovyo.Hata hivyo katika mahojiano na Bongo5, 20 Percent amekanusha kuzinguana na Afande na kuongeza kuwa hana uadui wowote na msanii huyo ambaye jina lake ni Seleman Msindi.

“Mimi na Afande Sele hatujawahi kuzinguana Zanzibar japo labda yeye kwa sababu zake binafsi alinizingumzia tofauti na watu wengi walishawahi kuniuliza hilo swali,” alisema 20. “Tuko kawaida tu kama watu tunaoweza kufanya kazi pamoja kama tulivyokuwa tunafanya zamani.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents