Bongo5 Exclusives

20 Percent azungumzia mipango mikubwa baada ya kupatana tena na Man Walter

Mshindi wa tuzo tano za muziki za Kilimanjaro 2011, Abbas Kinzasa ‘Twenty Percent’ amesema ameamua kurudi kwa prodicer wake John Shariza, maarufu kwa jina la Man Walter ili kuwaburudisha mashabiki ambao wanahisi kuna kitu wanakosa.
page

20% ameiambia Bongo5 kuwa kuungana tena na Man Walter ni kwaajili ya kuwarudisha mashabiki ambao imani zao zinawapa 20% na Man Walter kutokuwa pamoja zinasababisha mashabiki wa muziki kukosa burudani.

“Tumerudi ili mradi kuweka sawa mambo watu wataanza kufurahia ile combination ya ukweli,ingawa bado hatuna mkataba ni kama tunafanya kazi hasa kazi tu.Kutokana ni muda mrefu umepita kuna ngoma inakuja inaitwa ‘Subira yavuta heri’kwahiyo baada ya hapo wataendelea kupata ngoma nyingine zaidi kutoka kwa Man Walter na 20%,” alisema.

“Kwa upande wa filamu wasubiri filamu mwezi wa kwanza inatoka inaitwa ‘Lazima ajitambue kwanini haujitambui’ ambayo izungumzia mazingira ya maisha na muziki kama ilivyokuwa filamu yangu ya kwanza. Filamu yangu ya kwanza imenifanya niweze kuongeza mashabiki, imefanya watu waamini naweza kufanya vitu vingi na vyote vipo kwenye damu ndiyo maana ninafanya vizuri,” aliongeza msanii huyo.

“Mimi na Man Walter tuna fanana,kwasababu nasema Man Walter anakipaji na mimi nina kipaji lakini vipaji vyetu lazima vivaane tunaweza kutoa kitu kimoja.Katika kipindi ambacho mimi na Man Walter tumekosana n ikipindi ambacho Man Walter anapigiwa kelele za kushangiliwa na mimi napigiwa kelele za kushangiliwa yaani kwamba ni mastaa.

Ni wakati ambao ni mgumu sana kwa mtu ambaye anashika ile nafasi yaani ni staa, unaweza ukapotea njia unaweza ukafanyaje.Lakini wewe huwezi kuliona hilo ila yule mtu ambaye amekaa pembeni kama mkumbwa wako,pengine alivutiwa na kazi zako, basi akawa anaangalia maendeleo yako ya kazi hataki upotee, hataki uteleze. Kwahiyo anaangaliwa pale ambapo uliteleza, wapi ambapo pakirekebishika wewe unaweza kurudi katika hali yako ambayo inatakiwa uwe.

Ndio watu ambao walikaa wakaona kuna uhumimu wakutii hizi kiu za wanajamii ambao wanawazunguka Man Walter na 20%, na je? 20% na Man Walter kuna nini kinawazunguka mpaka wakose maziwa,wakose maji,wakose juice? Kuna watu ambao wana hekima zao, mimi naita wenye busara zao wakakaa chini wakasema kuna kila sababu za hawa watu, kukaa pamoja na kufanya kazi. Sasa mtindo wa kazi ndio kitu ambacho kinatakiwa kukaa chini,aina gani ya kazi ni milolongo gani ya kazi ,jinsi kazi itakavyokwenda bila kusumbuana. Maybe wameona wapi tulipokosea ndio maana kila kitu kinaenda kwa process.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents