Steven Kanumba: 40 Days since his passing, mystery still surrounds his death

Today marks 40 days since the veteran Tanzanian actor, Steven Charles Kanumba passed away. It is said that the actor sustained a head injury after slipping and falling, which as reported by the Coroner resulted in loss of oxygen supply to the brain and finally death.

The famous actor was said to have been in his home at Sinza Vatican, in the company of his alleged girlfriend, fellow actor Elizabeth ‘Lulu’ Micheal. The scenario painted thus far is one where these secret lovers had a misunderstanding which lead to a physical altercation that left Kanumba dead and Lulu, whom as it turns out is only 17 years old, fleeing the scene in panic.
Continue reading

Breaking News: Patrick Mafisango wa Simba SC Afariki Dunia.

Mchezaji Patrick Mafisango,amefariki dunia alfajiri baada ya gari alilokua anaendesha kupata ajali.

Kwa taarifa tulizozipokea, mchezaji huyo nguli ambaye ni raia wa Rwanda mwenye asili ya Congo, alikua anakwepa baiskeli mitaa ya Chang’ombe jijini Dar es salaam na ndipo akaingia kwenye Mtaro na gari na kufariki papo hapo.

Bongo5 inafanya jitihada za kupata taarifa za msiba kutoka kwa familia ya ndugu Mafisango ambapo tutazidi kuwahabarisha.

Taarifa hizi zimekuja kama pigo kubwa kwa wadau wapenzi n mashabiki wa mpira na wa mchezaji huyo, na mchezo huo umepoteza mcheaji mahiri.

Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi.

Picha ya Bushoke iliyozua Gumzo hii hapa

Baada ya msanii wa filamu na muziki wa bongo Flava Hemedi kumtupia wingu Bushoke na kusema alimuona Bushoke akiwa kwenye pozi la picha liliomletea hisia tofauti na kana kwamba Bushoke hayuko sawa, Bongo5 ilitinga kwenye file zetu na kuikuta picha ya Bushoke ambayo imeleta gumzo jijini.

Picha hii ambayo ilipigwa miaka kadhaa iliyopita inamuonyesha Bushoke katika enzi zake za kuanza muziki akiwa na swagga tofauti kidogo najinsi ambavyo yuko leo.

Wadau wengi kwenye industry wameipokea picha hii kwa hisia tofauti huku wengi wakiwa wanamshangaa msanii huyo wa longtime hit ‘Barua’.

Wadau mnaionaje?

Mama yake Rihanna ahamia kwa mtoto wake kwa kumhofia maisha yake

Maisha ya Good girl gone bad yameonekana kuchukua mkondo huo huo baada ya msanii huyo wa Kundi la Jay Z la Roc Nation kuonekana kufikia nafasi ya kua out of control kwa kula bata na kuzidisha unywaji.
Marafiki na sasa familia ya Rihanna waliokaribu naye wameonyesha wazi kutokubaliana na mwenendo wa Rihanna wa kuonekana club kila siku na kunywa pombe kupindukia, na kupelekea kulazwa hapa juzi kati kwa kutokupumzisha mwili wake inavyopasa.
Rihanna anasemekana kufuata tabia ya marehemu Whitney Houston kwa kutumia hata madawa ya kulevya na mpaka sasa wote waliokaribu naye wanamhimiza aende kupata usaidizi wa madaktari kumsaidia kuachana na masuala hayo.

Mama wa star huyo ameamua kuvalia ishu hii njuga na kuhamia nyumbani kwa Rihanna mjini Los Angeles ambapo atajaribu kumkanya na kumdhibiti mienedo ya mtoto wake huyo mwenye miaka 25.

Rihanna amedai kushangazwa na haya yote na kukanusha kwamba maisha yake yanaelekea pabaya wa kusema, yeye ni kijana mdogo na anaenjoy maisha yake bila kupretend wala kujificha.

Ommy Dimpoz Kuzindua Single yake,’Baadae’ kiaina yake jumapili hii

Best Upcoming Artist wa Kilimanjaro Music Awards na mkali wa Nai Nai, Ommy Dimpoz, anatarajia kupiga show ya ukweli Jumapili hii kwa ajili ya kuzindua single yake mpya ya ‘Baadae’.

Akizungumza na Bongo5, meneja wa msanii huyo, Muba, amesema kwamba kwa sasa Ommy yuko busy anamalizia kupiga show za Kili Winners Tour ambapo ameshazuguka mikoa mingi ya Tanzania akikamua na washindi wenzake, na punde tu atakapomaliza mwishoni mwa wiki hii show yake ya Mbeya, atakamua Bilz kiania yake.

Ommy Dimpoz atasindikizwa na wasanii wenzake Ben Pol, mwandani wake Diamond Platnumz na wasanii wengine wengi.

Usimose super handsome jumapili ya tarehe 20 kule Bilz mtu wangu.

Lady Gaga apigwa marufuku kukanyaga Indonesia

Msanii anayesifika kwa utofauti wake kimavazi na kimuziki Lady Gaga amepigwa marufuku na Serikali ya Indonesia kupiga show nchini humo kwa sababu zinazosemekana ni za kimaadili na kidini.

Lady gaga ambaye alishauza ticket zaidi ya elfu hamsini amelazimika kuifuta show hiyo baada ya kunyimwa kuingia nchini humo kwa madai kwamba anavaa kinyume na maadili ya nchi hiyo na yale ya Kiislam na zaidi mfumo wake wa kucheza utaweza kupelekea kuwaharibu wananchi wa Indonesia kwa kuwafunza yasiyokubalika kijamii nchini humo.

Lady Gaga hajatoa tamko lolote kufuatia kufutiwa visa ya kuingia nchini humo ila serikali hiyo imebaki kusisitiza hawawezi kumruhusu kuingia nchini humo,na si yeye tu bali ni msanii yeyote wa kigeni ambaye anaweza kutishia ukiukaji wa maadili nchini humo.

Wananchi wa Indonesia ambao walikua wamenunua tickets za show hiyo wamesikitika na kutaka serikali kutokubaki nyuma na kufungwa pigu za udini na kukandamizwa na wachache na kutoskikiliza matakwa ya wengi.

Wadau mnaionaje?

Wasanii wa Tanzania kupata shavu Italy

Baraza la Sanaa la Taifa kuptia wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo limepokea taarifa ya wasanii wa Tanzania kutakiwa kushiriki Maonyesho ya 16 ya sanaa za Kimataifa yatakayofanyika Mjini Rho, Italia kuanzia tarehe 3 hadi 11 Mwezi December 2011.

Kwa mujibu wa katibu mtendaji wa Basata Bwana Materego, maonyesho hayo yatalenga bidhaa za asili na za kiutamaduni kutoka nchi mbalimbali duniani zikiwemo za asili (typical products) , Muziki (Musical events), Ngoma (Dances), Mapambo (colours) na vyakula (flavours) ambazo kwa ujumla wake zinaelezea historia ya nchi na watu wake.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari Bwana Materego alisema Baraza linahimiza vyama na mashirikisho ya sanaa, wasanii na wadau wa sanaa kutumia fursa hii kuonyesha kazi mbalimbali za sanaa katika tamasha hilo.

Kwa maelezo zaidi juu ya maonyesho haya, wasanii na wadau wa sanaa watembelee tovuti ya
www.artigianoinfiera.it au kuwasiliana na waandaaji kupitia barua pepe cratfsfair@gestionefiere.com

Jay Z na Will Smith waungana na Obama kuhusu ndoa za jinsia moja


Jay-Z na Will Smith wameunga mkono tamko la Barack Obama kukubali ndoa za jinsia moja nchini Marekani, tamko ambalo lilipokelewa kwa hisia tofauti nchini kwa na kwengine duniani.

Will Smith alisifia tamko la Obama kuwa ni la kijasiri katika mwaka wa uchaguzi nchini Marekani, na aliendelea kusema kwamba ni jambo la kuunga mkono mtu yoyote akipata mwenzake wa kuwapenda na kuwasaidiana katika maisha.

Kwa upande wake Jigga alisema anaamini kuwa wapenzi wa jinsia moja wanapaswa kuwa na haki ya kuoana, na kwamba kinachofanyika majumbani mwao si suala lao wenyewe.

Jose Chameleon Only East African to perform at the 2012 London Olympics

Jose Chameleone is set to perform at the opening ceremony of the 2012 Olympic Games in London. He has been booked for this through the South-Africa based AS Entertainment. The latter company booked Jose Chameleone to perform at the 2010 World Cup in South Africa.
The company is still negotiating on how much money Jose Chameleone will be paid to perform come 2012. Chameleone might be the only singing representative from East Africa to perform at the London 2012 Olympics.
London 2012 Olympics games are scheduled to start on 25 July at 16:00 – 20:45 with two football matches of Women’s preliminaries at Millennium Stadium, Cardiff.

Airtel yazindua SUPA 5, yaleta ofa 5 kabambe kwenye Kuwasiliana, SMS na Intaneti

Airtel Tanzania imezindua ofa 5 kabambe zitakazowafaidisha wateja wake wanaotumia huduma zao za Intaneti (Data) pamoja na huduma ya kawaida ya kuongea na simu pamoja na ile ya kutuma ujumbe mfupi yaani SMS. Kati ya ofa mpya ziliyozinduliwa ni pamoja … Continue reading

King Majuto haumwi, msikubali kuchangishwa kwa ajili yake!


Leo tumepata taarifa kutoka kwa mke wake King Majuto kwamba mume wake haumwi ila kuna watu wanaochangisha kwa ajili yake. Kwa mujibu wake huo ni utapeli na anahofia ifikapo siku watahitaji kweli msaada ya watu watakosa kutokana na utapeli huo.

Kwa kweli we hope kwamba siyo kweli, kwa sababu kugeuza uhai wa mtu kuwa mradi wa kuishi mjini ni kitu kibaya sana.